Wandani wa Rais Uhuru waingia serikalini katika mageuzi ya baraza la mawaziri

  • | NTV Video
    5,623 views

    Wandani wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta sasa wamo serikalini. Katika mageuzi ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jioni hii ni kwamba mutahi kagwe ameteuliwa katika wizara ya kilimo huku aliyekuwa gavana wa kiambu william kabogo akiteuliwa kuwakilisha wizara ya teknolojia na mawasiliano. lee kinyanjui ameteuliwa katika wizara ya biashara, uwekezaji na viwanda.wengine walioteuliwa ni pamoja na margaret nyambura ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa ghana, aliyekuwa waziri wa michezo wakati wa uhuru ababu namwamba ameteuliwa kama mwakilishi wa kenya- unep, balozi dorothy angote ameteuliwa kuwa balozi wa zimbabwe huku dkt. andrew karanja akiteuliwa kama balozi wa brazil. salim mvurya ameteuliwa katika wizara ya michezo na vijana huku kipchumba murkomen aking'olewa kwenye wizara ya michezo na kuteuliwa katika wizara ya usalama wa ndani. ndiritu muriithi ameteuliwa kama mwenyekiti, bodi ya kra, anthony mwaura mwenyekiti, bodi ya kerra na kembi gitura - mwenyekiti, bodi ya hospitali ya k.u. mabadiliko haya yanajiri siku chache baada ya rais william ruto kukutana na rais mstaafu uhuru kenyatta.

    Subscribe to NTV Kenya channel for latest Kenyan news today and everyday. Get the Kenya news updates, discussions and other exciting shows.

    Website: ntv.nation.co.ke || Paper: Daily Nation || Twitter: @ntvkenya || Facebook: NTV Kenya || Instagram: NTV Kenya