Aliyekuwa gavana wa Meru asema atawania ugavana wa Meru tena mwaka wa 2027

  • | Citizen TV
    1,385 views

    Aliyekuwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza , amevunja kimya chake na kusema kuwa atasafisha jina lake na kukutana na wapinzani wake kwenye debe katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Kulingana na Kawira, mahasimu wake wa kisiasa wana taasubi ya kiume na walihakikisha ameondolewa mamlakani na kuhujumu haki yake ya kikatiba.