Naibu Kindiki atoa onyo kali kwa viongozi ambao wamekuwa wakikosoa serikali

  • | K24 Video
    426 views

    Naibu rais Profesa Kithure Kindiki ametoa onyo kali kwa viongozi ambao wamekuwa wakikosoa serikali akisema kwamba utawala hautakaa kimya na kuruhusu umma kupotoshwa kwa uongo na maneno yenye lengo la kuleta mgawanyiko. Akizungumza katika kaunti ya Embu, Kindiki pamoja na viongozi wengine walisisitiza kuwa serikali inafanya kila iwezalo kutekeleza ahadi zake kwa wakenya.