Serikali Yachukua Hatua Kulinda Wakulima Dhidi ya Kemikali Hatari

  • | K24 Video
    98 views

    Katika juhudi za kuhakikisha usalama wa wakulima na watumiaji wa mazao yao, serikali imeanza kuchukua hatua kali dhidi ya matumizi ya kemikali hatari, ikiwemo zile zinazotumika kwenye kilimo cha miraa. Waziri wa Kilimo, Mutahi Kagwe, ameagiza uharibifu wa zaidi ya magunia 20,000 ya mbolea bandia, akisisitiza kuwa serikali imejitolea kuwalinda Wakenya dhidi ya bidhaa zenye madhara. Hata hivyo, mashirika kadhaa katika sekta ya kilimo yameonya kwamba kupiga marufuku baadhi ya pembejeo kunaweza kuathiri uzalishaji wa mazao nchini.