Waititu anyimwa dhamana

  • | Citizen TV
    7,007 views

    Mahakama Kuu imekataa kumwachilia kwa dhamana aliyekuwa Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu, ambaye anasubiri kusikizwa kwa rufaa aliokata dhidi ya uamuzi wa kumfunga gerezani kwa kushiriki ufisadi. Katika Uamuzi wake Jaji Lucy Njunguna alisema Waititu hajawasilisha sababu za kutosha za kutaka kuachiliwa. Badala yake, mahakama imeelekeza rufaa yake isikizwe kwa haraka. Waititu alikuwa ameomba kuachiliwa kwa dhamana, akitaja matatizo ya kiafya kama mojawa ya sababu zake. Hata hivyo, katika uamuzi wa leo, mahakama ilisema magereza yana uwezo wa kutoa huduma za afya, na ikiwa kuna tatizo kubwa la kiafya, wafungwa hupelekwa katika hospitali za rufaa.