Wakaazi wasio na vitambulisho wasajiliwa Nakuru

  • | Citizen TV
    274 views

    Wakaazi wa kaunti ya Nakuru ambao Kwa miaka mingi wameishi bila vitambulisho kwa kutopita msasa wa kiusalama leo wanasajiliwa kwa vitambulisho eneo hilo. Wengi wa wanaohusishwa kwenye zoezi hili ni wale wanaotoka maeneo ya kaskazini mashariki. Zoezi hili likifuatia agizo la Rais William Ruto kuondoa zoezi la kuwapiga msasa wakaazi wa maeneo ya mpakani kabla ya kupata vitambulisho.