Rais Ruto apongeza KWS kwa kuweka huduma kidijitali

  • | KBC Video
    359 views

    Rais Dkt William Ruto amelipongeza shirika la huduma kwa wanyamapori humu nchini-KWS kwa kuweka huduma zake kwenye mfumo wa kidijitali, na kuongeza mapato yake kwa kiwango kikubwa. Kiongozi wa taifa alisema shirika hilo sasa linaweza kutumia mgao wake wa bajeti kwa asilimia-87, hatua ambayo imeiwezesha kutekeleza miradi yake mikuu na shughuli zake kwa jumla. Rais Ruto alisema hayo wakati wa hafla ya kufuzu kwa maafisa 1,274 wa ulinzi wa wanyamapori katika chuo cha shirika la KWS huko Manyani, kaunti ya Taita-Taveta. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive