Goma DRC: SADC wakutana huku M23 wakiendeleza mashambulizi

  • | BBC Swahili
    45,900 views
    Viongozi wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika SADC wanakutana mjini Harare, Zimbabwe katika kikao cha dharura kujadili mzozo unaoendelea kutokota mashariki mwa DRC. Haya yanajiri huku kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda likiendelea kupiga hatua ndani ya taifa hilo. Baada ya kuuteka mji wa Goma katika eneo la Kivu Kaskazini, sasa wanaendeleza mpango wao wa kuingia Kivu Kusini.