Hisia mseto kuhusu tangazo la Rais la kutangaza bonasi kwa wakulima wa miwa

  • | K24 Video
    117 views

    Januari 20 mwaka huu itasalia siku ya kihistoria kwa wakulima wa miwa. Hii ni baada ya Rais William Ruto kuwafuta jasho wakulima hao. Ilikuwa mara ya kwanza kwa wakulima kutangaziwa bonasi ya shilingi milioni 150. Tangazo hilo liliibua hisia mseto kutoka kwa viongozi, wakulima na wenyeji wa magharibi mwa kenya ambako kuna wakulima wanaonufaika na kiwanda cha Mumias.