Mauzo ya nyama ya punda yaongezeka Embu, Kitui, Machakos

  • | KBC Video
    26 views

    Wadau mbalimbali wakiwemo wale wa idara ya polisi, mashirika ya jamii na watetezi wa haki za wanyama wametoa wito wa kupiga marufuku uuzaji,ununuzi na usafirishaji wa nyama ya punda ili kuwanusuru wanyama hapo walio katika hatari ya kuangamia. Akiongea mjini Kithyoko kwenye mpaka kati ya kaunti za Machakos na Kitui baada ya mkutano wa kutathmini usalama wa punda, wadau hao walilalamikia ongezeko la visa vya punda wanaochinjwa na nyama yao kuuzwa bila idhini .Uchinjaji wa mnyama huyo unasemekana kutekelezwa misituni na nyama hiyo kuuzwa katika kaunti za Kitui , Embu na Machakos .Pia wametoa wito wa uhamasisho kwenye jamii kuhusu umuhimu wa mnyama huyo hususan katika maeneo kame .

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive