SADC na EAC kukutana kuhusu vita vya Goma, DRC

  • | BBC Swahili
    12,520 views
    Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitaandaa mkutano wa pamoja Ijumaa na Jumamosi wiki hii kuzungumzia mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mkutano huo utafanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania, taifa ambalo ni mwanachama wa jumuiya zote mbili - SADC na EAC. Hatua hii inafuatia makubaliano kati ya mwenyekiti wa SADC Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, pamoja na mwenyekiti wa EAC Rais William Ruto wa Kenya. Taarifa kutoka Ikulu ya Nairobi inasema kwamba Rais Felix Tshisekedi wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda wamethibitisha kushiriki mkutano huo, pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.