Stars yabanwa na Stallions

  • | Citizen TV
    392 views

    Timu ya taifa Harambee stars ilibanwa sare ya bao moja na Burkina Faso kwenye mechi yao ya kwanza ya mchuano wa mapinduzi usiku wa jana.

    Stars walianza vyema mchezo huo na kupata bao la kutangulia kupitia kwa winga wa KCB james kinyanjui aliyeunganisha mpira uliopanguliwa na kipa wa burkina faso mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Aboubakar Traore aliwasawazishia Burkina Faso dakika za lala salama za mchezo huo. Harambee stars sasa watavaana na tanzania siku ya jumanne.