Trump: Marekani itaidhibiti Gaza

  • | BBC Swahili
    5,318 views
    Rais wa Marekani Donald Trump amezungumzia mpango wake wa Marekani 'kuudhibiti mji wa Gaza', katika kile ambacho kingekuwa mabadiliko makubwa zaidi katika sera ya Marekani kuelekea Mashariki ya Kati katika kipindi cha miongo kadhaa. Akihutubia mkutano wa wanahabari, akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Trump alisema anaamini eneo lote la Gaza linafaa kujengwa upya, na Wapalestina wapelekwe sehemu nyingine.