Mpango wa maabara za kidijitali shuleni kupingwa na wadau wa elimu

  • | K24 Video
    124 views

    Juhudi za serikali kupitia wizara ya elimu kulenga kujenga maabara ya kubuniwa mitandaoni yaani virtual katika shule za sekondari zimepata pigo baada ya wadau katika sekta ya elimu kupinga mfumo huo. Waliopinga wamesema mfumo huo utachangia ubaguzi wa shule na wanafunzi ikizingatiwa kwamba shule nyingi nchini hazij wekeza katika maswala ya teknolojia. Wadau hao hata hivyo wameshinikiza kuimarishwa kwa elimu ya gredi ya 10 sawia na serikali kutoa mgao wa fedha kwa shule kwa wakati unaofaa .