Francis: Papa kutoka Amerika ya Kusini ambaye alilibadilisha Kanisa Katoliki

  • | BBC Swahili
    5,494 views
    Papa Francis jina lake kamili ni Jorge Mario Bergoglio, alikuwa Kardinali wa Argentina, na alikuwa na umri wa miaka sabini alipokuwa Papa mwaka 2013. Alikuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika na kutoka Ulimwengu wa Kusini. Alimrithi Benedict XVI, ambaye alikuwa Papa wa kwanza kustaafu kwa hiari baada ya takribani miaka 600. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani amefariki dunia Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake ya Casa Santa Marta, Vatican. Haya ni baadhi ya aliyoyanya kimataifa tangu alipokuwa Papa 2013 #bbcswahili #roma #papafrancis Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw