Mambo ya kukumbukwa aliyoyaacha Nyota wa NBA marehemu Mutombo

  • | VOA Swahili
    84 views
    Angalia mahojiano haya aliyofanya Mwandishi wa VOA Roger Muntu na Nyota wa NBA Dikembe Mutombo Marekani, Juni 07, 2021.⁣ ⁣ Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu wa NBA Dikembe Mutombo, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa safu ya ulinzi katika historia ya NBA na balozi wa muda mrefu wa kimataifa wa mchezo huo amefariki dunia Jumatatu (Septemba 30, 2024) baada ya kuugua ugonjwa wa saratani ya ubongo. Alikuwa na umri wa miaka 58.⁣ ⁣ Familia yake ilieleza miaka miwili iliyopita kwamba Mutombo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alikuwa anapatiwa matibabu huko Atlanta kutokana na uvimbe kwenye ubongo. NBA ilisema alifariki dunia akiwa amezungukwa na familia yake.⁣ ⁣ Dikembe Mutombo alikuwa mkubwa kuliko maisha, Kamishna wa NBA Adam Silver alisema. Uwanjani alikuwa mmoja kati ya walinzi wakuu bora kuwahi kutokea katika historia ya NBA. Akiwa nje ya uwanja alitumia muda wake kuwasaidia wengine.⁣ ⁣ Mutombo alicheza misimu 18 kwenye ligi ya NBA, akitokea chuo kikuu cha Georgetown na alichezea timu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Denver, Atlanta, na Houston.⁣ ⁣ Mutombo alicheza mara ya mwisho msimu wa mwaka 2008-09, akitumia muda wake baada ya kustaafu kujishughulisha na masuala ya hisani na huduma za dharura. Alizungumza lugha tisa na alianzisha Wakfu wa Dikembe Mutombo mwaka 1997, akizingatia kuboresha afya, elimu na ubora wa maisha kwa watu wa Congo.⁣ ⁣ ⁣ ⁣ ⁣ #mpirawakikapu #mchezaji #nyota #dikembemutombo #marekani #drc #voa #voaswahili - - - - - VOA Swahili inarusha matangazo ya Duniani Leo kupitia Tovuti yetu na jukwaa la Facebook Jumatatu hadi Ijumaa tukikuletea habari mbalimbali za siasa na uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili. Tembelea tovuti yetu voaswahili.com/duniani-leo na Makala Maalum ya Jarida la Wikiendi. Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu. Matangazo yetu yanasambazwa kupitia satellite, cable, FM na MW, na and kupitia mtandao wa vituo vya matangazo vya washirika wetu takriban 3000. Tangu kuanzishwa mwaka 1942, Sauti ya Amerika imeendelea na azma yake ya kutoa habari za kina na kuwaambia wasikilizaji wake ukweli. Tangu kipindi cha Vita Vya Pili vya Dunia, Vita Baridi, Vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na juhudi za ukombozi duniani kote hivi leo VOA imekuwa mfano katika kutekeleza kanuni za vyombo vya habari huru. Jiunge na VOA Swahili: » Tembelea Tovuti Yetu: https://bit.ly/3PtyNWc »Angalia Video Zaidi za VOASwahili: https://bit.ly/3TNTiiI »Pakua VOA+ katika vifaa vya Apple : https://bit.ly/VOAPlus »Download VOA+ katika vifaa vya Android https://bit.ly/3KykriI »Tembelea Tovuti yetu: https://www.voaswahili.com/ »Upende ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/voaswahili »Tufuatilie katika Instagram: https://www.instagram.com/voaswahili »Tufuatilie katika X: https://twitter.com/voaswahili »Tufuatilie katika YouTube: https://www.youtube.com/@VOASwahili