Wagonjwa zaidi waendelea kuugua South Mugirango

  • | Citizen TV
    378 views

    Visa zaidi vya wagonjwa vimeendelea kuripotiwa katika vijiji kadhaa vya eneobunge la South Mugirango, wakiugua ugonjwa usioeleweka. Wenyeji wa vijiji vya Amarondo, Nyarigiro na Nyabigege wanaendelea kuripoti wagonjwa zaidi. Hapo jana, katibu wa afya ya umma Mary Muthoni alisema maafisa wa afya wametumwa eneo hilo kutathmini hali. Hali hii imeendelea huku matokeo ya sampuli zilizochukuliwa na idara ya afya kaunti ya Kisii yakitarajiwa kwa hamu kutolewa hapo kesho, ili kubaini sababu ya wakaazi kuugua ugonjwa huu na chanzo chake