Wakaazi wa Akingli kaunti ya Kisumu walalamikia kuhangaishwa na nyani

  • | Citizen TV
    319 views

    Wakazi wa kijiji cha Akingli kaunti ya Kisumu sasa wanalitaka shirika la wanyapori KWS kuregesha mitego ya nyani iliyoondolewa kijijini humo mwaka jana ili kuwaepushia kero la wanyama hao.Wakazi hao wanalilia hasara baada ya ongezeko la nyani wanaovamia mashamba yao, na hata kuwatishia watoto wanaoenda shuleni machweo. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, shamba nyingi sasa zimesalia bila mazao kutokana na kero la nyani.